Tatumzuka | Home
Title

TatuMzuka vigezo na masharti

Cheza TatuMzuka




Toleo kuanza kutumika Rasmi Julai 26 2017



UTANGULIZI

The Network Ltd ni kampuni iliyosajiliwa kwa mujibu wa sheria za Tanzania Bara (namba ya usajili 103194) ambayo anwani yake ya usajili ni Mikocheni B, Nyumba Namba 35. Dar es Salaam, Tanzania.

The Network Ltd imeruhusiwa na ipo chini ya mamlaka ya Bodi ya Michezo ya Bahati Nasibu Tanzania (inayotambulika kama GBT) chini ya sheria ya Bahati Nasibu Namba 4 ya 2003, leseni Namba OCL000000005

Mchezo huu wa Droo ya TATU MZUKA uko kwa mujibu wa vifungu vya Sheria ya Mchezo wa Bahati Nasibu ( Sheria Na. 4 ya 2003) na tatizo lolote litakalojitokeza litatatuliwa kwa mujibu wa vifungu vya sheria hii.

Kanuni zifuatazo za Michezo ya droo ya TATU MZUKA inayochezwa mtandaoni au kupitia simu ya mkononi au kibobwezo (kanuni hizi) zitatumika wakati wa kucheza mchezo wa droo wowote mtandaoni au kupitia simu ya mkononi au kibobwezo. Kila mchezo wa droo ya TATU MZUKA utakuwa na taratibu zake ambazo zitatumika, na baadhi ya michezo ya droo ya TATU MZUKA pia itakuwa na kanuni zake maluumu za kimchezo ambazo zitatumika kila baada ya muda.

Huu Mchezo wa droo ya TATU MZUKA unafahamika pia kwa lugha ya Kiingereza kwa jina la ‘Pick 3 Draw Game’. Majina yote ni sawa na yanaweza kutumika kwa maana moja kwa madhumuni ya nyaraka hii.

Mkataba huu unaweka vigezo na mashariti ya mahusiano ya makubaliano kati ya The Network Ltd na wewe kama mchezaji. Vigezo vitatumika kwenye Bahati Nasibu kupitia huduma za simu, ujumbe mfupi wa simu, pesa kwa njia ya simu, na vibobwezo vingine vyote vilivyounganishwa. Utapaswa kukubaliana na vigezo hivi na mashariti yote katika kipindi chote cha mahusiano. Kampuni itakuwa na haki ya kufanya mabadiliko kwenye vigezo na masharti muda wowote na bila kutoa taarifa ya awali. Juhudi za makusudi zitafanywa kuwataarifu wachezaji kuhusu maboresho ya msingi yaliyofanywa kwenye vigezo na masharti. Bila kuathiri vigezo na masharti, litakuwa ni jukumu la mchezaji kufatilia mabadiliko yote yaliyofanyika na itachukuliwa kwamba kwa kucheza, wachezaji wote wamesoma, wameelewa, na wamekubaliana na vigezo na masharti yote.

Maelezo ya Mchezo wa TATU MZUKA.

TATU MZUKA ni mchezo wa droo uliojikita kwenye kuchagua seti tatu ya namba ambazo zitajumuisha ubashiri. Nafasi ya kushinda itajumuisha namba kuanzia 0 mpaka 9. Wakati wachezaji wanaingiza namba, wanaweza kuchagua namba zao kupitia Mpesa au kupitia Mtandaoni.

Njia za kuingia kwenye Mchezo wa TATU MZUKA

  1. MTANDAONI:

Mchezaji anaweza ingia kwenye mchezo wa TATU MZUKA kupitia anwani ifuatayo:

tatumzuka.co.tz

Wachezaji wapya wanatakiwa kujisajili kabla ya kubahatisha.

Wachezaji wenye akaunti Sahihi wanaweza cheza Bahati Nasibu kwenye mchezo wa TATU MZUKA kwa kuchagua kati ya njia zifuatazo:

Chaguo la bahati: namba zitachezeshwa bila kufuata mpangilio maalumu kwa niaba ya mchezaji.

Chaguo la Namba: mchezaji anaweza chagua namba zake kwa ajili ya kucheza mchezo wa TATU MZUKA

Notisi:

  1. Tigo Pesa, Vodacom- Mpesa, na Airtel Money ni mitandao ya simu pekee ambayo huduma zake za kifedha zinazotumika kwa sasa.
  2. Kwa wachezaji wapya, taarifa za akaunti na matangazo kupitia ujumbe mfupi wa maandishi unaohusu akaunti utatumwa kupitia ujumbe mfupi wa maandishi katika hatua ya ubashiri wa kwanza.
  3. Mchezaji atawajibika kulipia makato yote yatakayokatwa kwenye kila muamala na waendeshaji wa mtandao wa simu husika.

  • 2. PESA KWA NJIA YA SIMU:

Wachezaji wanaweza kuingia kwenye mchezo wa TATU MZUKA kupitia akaunti za fedha za simu zao kwa Bahati Nasibu.

Bahati Nasibu kupitia simu, mchezaji lazima acheze walau kiwango kidogo cha pesa kisichopungua shilingi za Kitanzania 500/= kwenda namba ya Malipo 555111

Mchezaji lazima atumie akaunti au mfumo wa kifedha kwa njia ya simu kama njia ya kuingiza namba zake tatu alizochagua. Kushindwa kuingiza namba hizi kwa kuzingatia njia sahihi utaleta matokeo kwenye mfumo wa The Network Ltd kwa kutoa seti ya namba za bahati

Mchezaji atawajibika kwa muamala wowote wa kifedha unaohusiana na ubashiri.

Pale itakapothibitika kwamba muamala umethibitishwa mchezaji atatumiwa mkeka wa ubashiri wake kupitia ujumbe mfupi wa maandishi.

Notisi:

i. Tigo Pesa, Vodacom Mpesa, na Airtel Money ni mitandao ya simu ya kifedha ambayo inatumika kwa sasa.

ii.Kwa wachezaji wapya, taarifa za akaunti zao na uendelezaji wa ujumbe mfupi wa maandishi unaohusu akaunti utatumwa kupitia ujumbe mfupi wa maandishi katika hatua ya kwanza ya ubashiri.

iii.Mchezaji atawajibika kulipia makato yote yatakayokatwa kwenye kila muamala na waendeshaji wa mtandao wa simu husika.

1. 1. Kanuni za mchezo wa TATU MZUKA

1.1 Mchezo wa TATU MZUKA unahusisha droo isiyofuata utaratibu maalumu ya namba tatu za tarakimu kila moja ikichaguliwa kutoka 0 mpaka 9.

1.2 Droo inatumia utaratibu usio maalumu wa namba zilizozalishwa na kuthibitishwa na GBT.

1.3 Droo zimepangwa kila baada ya muda dakika 5. Mda wa droo halisi utategemea mchakato wa maingizo kama vile The Network Ltd inaweza kutimiza majukumu yake kwa GBT

1.4 Dau la mchezo wa Tatumzuka ni kati ya Tzs 500 na Tzs 30000. Licha ya ukomo wa kiwango huo, mchezaji anaweza kuomba kuondolewa kwa ukomo wa dau hilo kwa kuwasiliana na kitengo cha huduma kwa wateja. Tatumzuka ina mamlaka ya kukubali au kukataa maombi hayo kulingana na sera za mchezo na ufanyaji wake wa kazi.

1.5 Kwa kukosekana kwa maombi ya kuongeza dau, kama mchezaji atajaribu kucheza juu ya kiwango cha dau kilichowekwa, mchezaji atarudishiwa kiwango kilichozidi baada ya kutoa makato ya gharama za kufanyia muamala huo.

1.6 Kama mchezaji anataka kucheza/ Bahati Nasibu zaidi ya kiwango cha juu kilichowekwa cha Bahati Nasibu, watatakiwa kutoa taarifa ya dhamira/nia yao kwa The Network Ltd kupitia timu ya kituo cha huduma kwa wateja au tovuti

1.7 Dau litaonyeshwa kwenye sehemu inayohusika ya TATU MZUKA kwa mda wa ambao ubashiri utawekwa

1.8 Mwisho wa Bahati Nasibu kwa TATU MZUKA utaamuliwa na The Network Ltd na kwa sasa umepangwa kuwa mda wa sekunde 30 kabla ya droo, na utaonyeshwa kwenye tovuti.

1.9 Kuna njia mbili za kushinda. Aina za tuzo zimeanishwa hapa chini:

1.9 Kuna njia mbili za kushinda. Aina za tuzo zimeanishwa hapa chini:

a) Kwa kulinganisha namba 3 katika mlolongo(aina ya 1 ya tuzo)

b) Kwa kulinganisha namba 2 lakini sio namba 3 zote (aina ya 2 ya tuzo)

c) Kwa kulinganisha namba 3 bila mlolongo (Aina ya 3 ya tuzo)

1.10 Mchezaji anaweza kushinda tuzo moja tu kwa ubashiri mmoja atakaouweka, ambayo itakuwa ni kubwa katika makundi ya tuzo yaliyopo katika ubashiri uliofanikiwa, na yenye mahusiano na ubashiri wa TATU MZUKA.

1.11 Tuzo itakayolipwa kwa wachezaji kulingana na ushindi wa bashiri ya The Network Ltd. kupitia Tatu Mzuka utakuwa ni ule utakaotangazwa kwenye tovuti ya TATU MZUKA.co.tz kulingana na droo husika.

1.12 Nafasi za ushindi kwa kila njia 2 za ushindi ni kama ifuatavyo:

a) Kundi/Aina ya Tuzo ya 1: 1- njia 1 kwenye 1000

b) Kundi/Aina ya Tuzo 2: 3- njia 1kwenye 6.7

1.13 Matokeo yanawezwa kuangaliwa kwa kutembelea tovuti ya tatumzuka.co.tz. Matokeo haya pia yatatumwa kwa wachezaji wote waliobashiri kwenye mchezo husika.

1.14 The Network Ltd itajaribu kuhakikisha kwamba matokeo yanayoonyeshwa kwenye tovuti au yanayochapishwa kupitia vyanzo vingine yako Sahihi (ikiwa ni pamoja na Tuzo, Mchanganuo wa Tuzo na ushindi). Ingawa kila juhudi itafanywa kuhakikisha usahihi wa taarifa hii, The Network Ltd haitawajibika kisheria kwa makosa yeyote kutokana na taarifa hizo.

2. 2. Kanuni za kuingia

2.1 Unatakiwa kuwa na akaunti ya pesa kwa njia ya simu iliyosajiliwa kwenye akaunti yako na kuwa na fomu Sahihi yenye taarifa za utambulisho inayohusiana na akaunti ya pesa kwa njia ya simu Tanzania.

2.2 Kila bashiri lazima inunuliwe kwa bei yake kamili, isipokuwa maingizo ya bure yaliyogawiwa na The Network Ltd kwenye promosheni au kwa njia ya tuzo kwa kila mchezo wa TATU MZUKA.

2.3 Bashiri zitafanyika kupitia The Network Ltd tu.

2.4 Kama bashiri itafanyika baada ya siku ya mwisho ya droo iliyowekwa (kama ilivyotangazwa kwenye Tovuti) , bashiri hiyo moja kwa moja itaingizwa kwenye droo inayofuata.

a) Kama bashiri imepokelewa baada siku ya mwisho iliyotangazwa, bashiri hiyo itaingizwa kwenye droo inayofuata.

b) Kama bashiri imepokelewa baada ya siku mwisho iliyotangazwa kutokana na kuchelewa kwenye mtandao au kutokana na mifumo ya kompyuta au haikuonekana kutokana na matatizo ya kiufundi, bashiri hiyo itaingizwa kwenye droo inayofuata

2.5 Bashiri yako itakuwa Sahihi kama itarekodiwa kwenye mfumo wa kompyuta wa The Network Ltd.

2.6 Ikitokea umeweka pesa kwenye akaunti ya pesa kwa njia ya simu kwenye The Network Ltd kukamilisha muamala wa Bahati Nasibu lakini kutokana matatizo ya kiufundi au tatizo lolote lile, The Network Ltd haitoweza kuthibitisha pesa yako uliyoiweka na kutoa ubashiri kwa mda huo, The Network Ltd itathibitisha pesa yako uliyoiweka na kutoa ubashiri kwenye droo inayofuata baada ya kurekebisha matatizo ya kiufundi..

2.7 Unaweza Bahati Nasibu na kupokea tuzo kwa mujibu wa kanuni hizi.

2.8 Hakuna haki ya jumla kwa mtu Bahati Nasibu. The Network Ltd inaweza kugoma kuruhusu bashiri kwa yeyote, na/ au kuweka ukomo wa idadi ya Bahati Nasibu.Unaweza kuweka, bila kutoa maelezo au sababu.

2.9 Kwa mujibu wa kanuni 2.8, watu wafuatao hawawezi Bahati Nasibu na The Network Ltd haitawajibika kisheria kulipa tuzo kwa wao:

a) Yeyote aliye chini ya miaka 18, hata kama mtu huyo anabashiri kwa niaba yao au yeyote.

b) Wakurugenzi na wafanyakazi wa The Network Ltd

c) Baadhi ya waajiriwa wa The Network Ltd kama vile wakandarasi wakuu au wakandarasi wasaidizi.

d) Wabia na watu ambao kwa Kiasi fulani, wanatunzwa na yeyote aliyetajwa kwenye kanuni 2.9(b) na 2.9(c) au kama ni kuishi wanaishi kwenye nyumba moja na mtu huyo.

e) Mtu yeyote aliye na akaunti yenye hadhi inayowazuia Bahati Nasibu au kupokea tuzo (pamoja na mtu ambaye akaunti yake imezuiliwa kwa mda au imefutwa).

f) Mtu yeyote The Network Ltd inaweza aamua nakuainisha kwenye marekebisho ambayo itafanya kwenye kanuni hizi au kwenye kwenye mchapisho mengine sahihi kila wakati/kila baada ya mda itakavyoona inafaa.

2.10 Kama tuzo italipwa kwa yeyote aliyetajwa kwenye kanuni 2.9, mtu huyo atatakiwa alipie tuzo hiyo haraka iwezekanavyo.

2.11 Baada ya GBT kukubali kwa maadishi The Network Ltd au wafanyakazi wa The Network Ltd wanaweza kucheza Bahati Nasibu kwa ajili tu ya kuthibitisha akaunti na kununua kwa kutumia akaunti ya pesa kwa njia ya simu. GTB inaweza weka masharti ya kufuata kabla ya kukubaliwa pamoja na, kwa mfano wafanyakazi wa The Network Ltd na The Network Ltd hawatastahili kunufahika na tuzo zilizoshinda kwenye bashiri hizo.

3. Majukumu yako

a) Hakikisha tiketi yako inaonyesha bashiri Sahihi, mchezo na tarehe ya droo; na

b) Kudai (pale inapobidi) na hakikisha unapokea Kiasi kamili cha Tuzo yeyote unayostahili.

c) Ikitokea kuna kodi itatakiwa kulipwa kutokana na tuzo, The Network Ltd itapunguza Kiasi hicho na kukipeleka kwenye mawakala wa ukusanyaji wa kodi. Washindi watapewa risiti za Malipo ya kodi hizo pale inapofaa.

4. Vigezo na Masharti ya Ushindi

4.1 Kama kuna bet itakayolinganisha namba za droo na dau la bet hiyo likawa ni la kiwango cha chini kabisa (kwa sasa shilingi 500). Jedwali lifuatalo linaonesha malipo yatakayofanywa kwa bet hiyo:

Dau

Milingano

Malipo

Mgawanyo

TZS 500

Linganisha namba 3 kwa mpangilio

100,000

Hapana

TZS 500

Linganisha namba 2

TZS 1,125

Hapana

TZS 500

Linganisha namba 3 bila mpangilio

TZS 50,000

Hapana

4.2 Kama kuna bet itakayolinganisha namba za droo na dau la bet hiyo likawa ni la kiwango cha juu kabisa (kwa sasa shilingi 30,000). Jedwali lifuatalo linaonesha malipo yatakayofanywa kwa bet hiyo:

Dau

Milinganyo

Malipo

Migawanyo

TZS 30,000

Linganisha namba 3 kwa mpangilio

TZS 6,000,000

Hapana

TZS 30,000

Linganisha namba 2 kwa mpangilio

TZS 67,500

Hapana

TZS 30,000

Linganisha namba 3 kwa mpangilio

TZS 150,000

Hapana

4.3 Kama bet italinganisha namba za droo na bet hiyo kuchezwa katika kiwango chochote cha dau

· Ikilinganisha namba mbili malipo yatakuwa ni mara 2.25 ya dau lililochezwa

· Ikilinganisha namba tatu malipo yatakuwa ni mara 200 ya dau lililochezwa

. Ikilinganisha namba tatu bila mpangilio ni mara 5 ya dau

4.4 KUMBUKA: Malipo ya kila ushindi yatakatwa kodi kwa kiwango cha wakati huo, kwa sasa ni 20%. The Network itawasilisha kodi TRA kwa kuzingatia matakwa ya sheria. Hii itakokotolewa kwenye malipo baada ya kutoa dau kisha kuzidisha na 20% na kiwango hiki kitatolewa kwenye kila ushindi katika hali zote.

4.5 The Network itachezesha droo za kila wiki ambapo namba tatu zitachukuliwa na mchezaji akiwa amecheza namba zozote TATU (mf akiwa amechagua namba hizo katika mpangilio wowote) kati ya hizo namba tatu za droo atapata nafasi moja ya kuingia kwenye droo ya zawadi kwa kila shilingi 500 iliyochezwa hadi wakati wa kufunga droo ya wiki. Baada ya droo kuchezeshwa, tiketi zote za wiki hiyo zitaisha muda wake na hazitakuwa na sifa tena.

4.6 Droo ya zawadi itaendeshwa kwenye muda maalum kama ilivyotangazwa kwenye mtandao www.tatumzuka.co.tz na itaendeshwa kwa usimamizi wa Bodi ya michezo ya kubahatisha Tanzania GBT. The Network itachagua tiketi bila utaratibu maalum kutoka kwenye rundo la tiketi. The Network itampigia simu mwenye tiketi, kama muhusika hatapokea simu The Network itampigia simu mchezaji anayefuata. Endapo atapokea simu, mhusika atapata nafasi ya kuingia kwenye mzunguko unaofuata pamoja na wachezaji wengine watatu huku wakiwa na nafasi ya kufikia zawadi kubwa zaidi.

4.7. Kampuni ya The Network Ltd itaendesha droo za automatiki ambapo namba tatu zitachaguliwa na mchezaji yeyote aliecheza namba zozote kati ya hizo tatu (yaani amecheza namba zote tatu katika mpangilio wowote) za droo atapata nafasi moja katika droo ya zawadi kwa kila shilingi 500 iliyochezwa ndani ya muda wa droo husika.

5. Kudai Tuzo

5.1 Unaweza kudai tuzo kama tu wewe ndiye mmiliki wa akaunti ya bashiri iliyoshinda.

5.2. Bashiri uliyotumiwa haiwezi tumika kama ushahidi wa bashiri au wa namba zilizo chaguliwa kwa mchezo au kutumika vinginevyo kudai tuzo wala uthibitisho wa manunuzi ulioonyeshwa au uliotumwa kwako na The Network Ltd hauwezi kutumika kwa hali yeyote kama ushahidi kwamba unastahiki Tuzo

5.3. Kama hautofuata hatua zilizowekwa kwenye kanuni 5.5, Tuzo zitadaiwa kabla ya mwisho wa siku 30 baada droo husika ( kipindi cha kudai) ukitumia hatua mojawapo ya zilizowekwa kwenye kanuni 5.4 stahiki yako kwenye Tuzo utaipoteza na tuzo haitalipwa kama Tuzo hiyo haitadaiwa ndani ya kipindi cha kudai labda kama utafuata hatua zilizowekwa kwenye kanuni

5.4. Kama unadai zawadi/tuzo ndani/katika kipindi cha madai, unatakiwa kuwasilisha madai kwa kutumia moja ya njia zifuatazo;

a) Kupitia Akaunti yako, kwa kuthibitisha kwamba malipo yanatakiwa yafanyike kwako. Hii inatakiwa ifanyike kabla ya saa tano usiku ya siku ya mwisho ya madai.

b) Kupitia simu ya timu ya watoa huduma kwa wateja. Unatakiwa kupiga simu kwa timu ya huduma kwa wateja ndani ya muda wa kazi ambao wakati wa kuandika taratibu hizi ni; Saa Mbili Asubuhi – Saa Mbili Usiku Jumatatu mpaka Jumamosi, na saa Tatu Asubuhi-Saa Kumi na Moja jioni kwa siku ya Jumapili- masaa ya kufungua yatapungua kwa siku za sikukuu za Krismass na Mwaka mpya. Unashauriwa kurejea katika tovuti kwa masaa ya kufungua kwa sasa.

c) Kuja mshindi mwenyewe katika ofisi za The Network Ltd’s katika muda wa kazi ndani ya kipindi cha madai. The Network Ltd ni lazima ipokee taarifa zinazojitosheleza kuthibitisha kua wewe ndio mmiliki wa akaunti ambayo ina ingizo la ushindi, pamoja na fomu ya madai iliyojazwa, na fomu nyingine zozote au nyaraka ambazo zitahitajika na The Network Ltd (pale inapofaa) *Ofisi za The Network Ltd kwa sasa zinapatikana Mikocheni B Nyumba namba 35, Dar es Salaam, Tanzania. Anuani ya ofisi inaweza ikabadilika. Muda wa masaa ya kazi ni; Saa Tatu Asubuhi-Saa Kumi na Moja na Nusu Jioni Jumatatu mpaka Alhamisi na Saa Tatu Asubuhi-Saa Kumi na Moja Jioni siku ya Ijumaa (isipokua Likizo za Kibenki). Muda wa kazi utapungua katika siku za Christmass na Mwaka mpya.

5.5 Tuzo itadaiwa na mshindi mwenyewe ndani ya siku saba tangu mwisho wa siku ya kudai zawadi hiyo kama, kabla ya mwisho wa kuwasilisha madai, mshindi aliwasiliana na kufahamisha The Network Ltd kwamba ana nia ya kudai tuzo/zawadi kwa namna hiyo (na anataja jina lake, anwani na taarifa zote za bashiri ambazo The Network Ltd watazihitaji) na pia kama utawasilisha uthibitisho wa utambulisho na fomu iliyokamilika ya madai ya tuzo inayohusika na mshindi katika ofisi za The Network Ltd katika muda wa kazi (tazama kanuni ya 5.4) ndani ya kipindi cha siku saba. Unaweza kuwasilian na The Network Ltd kupitia;

a) Kupiga simu kwa timu ya huduma kwa wateja katika muda wa kazi kwa wakati mbalimbali. Tazama hapo juu au rejea tovuti ili kujua muda wa sasa wa kufanya kazi wa timu ya huduma kwa wateja.

b) Kwa kutuma baruapepe help@tatumzuka.co.tz. The Network Ltd lazima ipokee baruapepe kabla ya kuisha muda wa kuwasilisha madai.

c) Kama utashindwa kudai ndani ya muda wa nyongeza wa siku saba, stahili yako ya tuzo utakua umepoteza na tuzo HAITALIPWA.

5.6. Unaweza kudai tuzo ya kiwango cha juu ambacho umebashiri na kushinda. Hautoweza kudai tuzo kwa tuzo ya kiwango cha chini, au kwa tuzo yoyote ambayo haukuidai katika droo ya zawadi.

5.7. Tuzo zote ambazo hazijadaiwa na washindi miezi mitatu baada ya kuisha kwa kipindi cha kudai, tuzo hizo zitasalimishwa GBT.

5.7. Tuzo zote ambazo hazijadaiwa na washindi miezi mitatu baada ya kuisha kwa kipindi cha kudai, tuzo hizo zitasalimishwa GBT.

6. Uhitaji wa kuhalalisha

Kabla ya Tuzo kulipwa katika bashiri, ni lazima ithibitishwe kikamilifu kwa mujibu wa taratibu za kuhalalisha zilizopo The Network Ltd kwa wakati husika. Maamuzi ya The Network Ltd juu ya bashiri kua halali au lah, itakua ya mwisho.

6.2. Bila kuzuia maelekezo ya kanuni ya 6.1, The Network Ltd itatamka bashiri kutokua halali (na haitalipa tuzo yoyote kuhusiana na bashiri husika) kama;

a) Bashiri ni matokeo ya kitendo chako au cha mtu mwingine ambacho kililenga kuongeza nafasi yako au ya mtu mwingine kushinda tuzo katika mchezo husika zaidi ya nafasi ya wachezaji wengine wa mchezo huo, au kuongeza tuzo hiyo; au

b) Bashiri itakua ya kughushi, yote au sehemu ya bashiri itakua ya kughushiwa, au bashiri imeshindwa kupita taratibu za kuthibitisha na za kiusalama wa The Network Ltd.

c) Dai la Tuzo halikupokelewa ndani ya muda wa kuwasilisha madai ulioainishwa katika kanuni ya 5.3 na 5.5;

d) Namba ya Tiketi ya bashiri haipo katika orodha rasmi ya The Network Ltd ya washindi, au tuzo husika ya mshindi wa utabiri huo wenye nambari ya tiketi husika iliyokwisha lipiwa awali; au

e) Taarifa zinazohusika na Tiketi namba ya bashiri hazioani na rekodi za The Network Ltd za nambari ya tiketi hio.

f) The Network Ltd inaamini kwamba bashiri/dau iliyonunuliwa na au kwa niaba ya mtu aliyeeelezwa katika moja ya kundi katika kanuni ya 2.8

6.3. Bila kuzuia/kuathiri maelekezo ya kanuni ya 6.1, The Network Ltd itatamka kua dau/bashiri ni batili (na haitalazimika kulipa tuzo yoyote) kama;

a) The Network Ltd inaamini kwamba mtu anaedai tuzo sio mmiliki wa akaunti husika au sio mwakilishi wa mtu huyo, au taarifa zilizotolewa na mtu anaedai tuzo hazijakamilika au zimerekebiswha au zimefinyangwa.

b) Bashiri/dau haijatolewa au kuuzwa na The Network Ltd.

c) Nambari ya Tiketi (au sifa nyingine za kipekee za bashiri) havioani na rekodi za The Network Ltd katika mfumo wake wa kompyuta kwa mchezo ambao bashiri inahusiana nao.

7. Malipo ya Tuzo

Taarifa ifuatayo inaonesha namna gani mchanganuo wa tuzo wa viwango tofauti inatakiwa kudaiwa na namna ya kulipwa.

a) Tuzo zinazoanzia kiwango cha Tsh 1000 mpaka Tsh 5,000,000: Tuzo na ushindi mwingine kutoka kwenye michezo katika kundi hili zitaingizwa moja kwa moja katika akaunti ya simu yako ya mkononi.

b) Tuzo ya thamani ya Tsh 5,000,000 mpaka Tsh 6,000,000: Tuzo na ushindi mwingine katika kiwango cha Tsh5, 000,000 mpaka 6,000,000 kutoka kwenye michezo ambayo inanunuliwa au kuchezwa kwenye simu ya mkononi itatakiwa kudaiwa na mshindi mwenyewe ambaye Tiketi ilitolewa, katika ofisi za The Network Ltd. Taarifa zaidi zinapatikana kwa kuwasiliana na ofisi za The Network Ltd kitengo cha huduma kwa wateja kwa 0659070070. Utakiri na kukubali kwamba utatakiwa kukidhi matakwa ya The Network Ltd juu ya madai ya Tuzo, ikiwa ni pamoja na kuthibitisha utambulisho pamoja na stahiki yako ya tuzo kadiri The Network Ltd itakavyojiridhisha kwa maamuzi yake binafsi. Utatakiwa kutoa fomu sahihi ya utambulisho yenye picha ya utambulisho na taarifa nyingine ambazo The Network Ltd inaweza kuzihitaji katika kuthibitisha una sifa ya kupokea tuzo.

7.2. The Network Ltd itakua na haki ya;

a) Kulipa tuzo kwa njia ya cheki, uhamisho kwa njia ya bank, salio la moja kwa moja au pesa kwa njia ya simu. Kama malipo yatafanyika kwa tuzo ya Tsh. 5,000,000 au pungufu, tuzo hio itawekwa (kwa gharama zako) katika akaunti ya simu yako uliyojisajiri katika akaunti yako au akaunti nyingine mtakayokubaliana kati yako na The Network Ltd.

b) Kukuomba kufika katika ofisi za The Network Ltd kudai tuzo yako

c) Kuzuia tuzo, kwa sharti kua wanazuia kwa nia njema mpaka pale itakapothibitika kua bashiri/dau ni halisi na pia madai yamefanywa kwa nia njema

d) Kuzuia tuzo (au kutaka kurudisha tuzo ambayo imekwishalipwa) mpaka pale ambapo uchunguzi mahususi uwe umefanyika, kama The Network Ltd ikiamini kwama kwa sababu za msingi kwamba mdai tuzo; hautambuliki kisheria kua yeye ndio mpokea tuzo; au kwamba tuzo ililipwa kwa mazingira ambayo The Network Ltd imeamua (kwa mujibu wa Kanuni ya 11.1) kwamba bashiri/dau sio halali au yenye dosari; au pale ambapo The Network Ltd ina sababu nyingine za msingi kuhoji kama una stahili kupewa tuzo. Ukaguzi na maulizo yoyote yatafanyika papohapo na The Network Ltd.Utatakiwa kulipa mapema pale ambapo The Network Ltd imekutaka kurudisha tuzo inayotakiwa kurudishwa.

e) Kurudisha tuzo ambayo ililipwa kimakosa katika akaunti yako

f) Kuomba uthibithisho wa stahiki ya tuzo (pamoja na, bila kuzuia taarifa za utambulisho, uthibitisho wa utambulisho na uwezo wa kudai)

g) Kukataa kulipa tuzo kama hutoweza au umeshindwa kutoa uthibitisho wa kujitosheleza wakati wa kudai tuzo hio. h) Kumpiga picha mtu yoyote ambae anadai tuzo kwa mujibu wa rekodi za The Network Ltd.

i) Kuiomba mahakama kutoa uamuzi juu ya nani anastahili kulipwa tuzo na/au kulipa tuzo hio mahakamani.

j) Kukataa kulipa tuzo kama umegoma kutia sahihi nyaraka zote unazotakiwa na mdhamini wa bima.

7.3. Haki ya kupokea tuzo haiwezi kuhamishika kwenda kwa mtu mwingine.

7.4. The Network Ltd. haitakuwa na wajibu au haitawajibika kisheria kwa mtu yeyote anaedai tuzo ambayo imekwisha lipwa kwa mtu aliyejifanya kutambulika kwa akaunti husika.

7.5. Hakuna riba itakakayolipwa kwa Tuzo yoyote, hii ni pamoja na bila kuzuia; wakati Ukaguzi na maulizo yoyote yakiwa yanafanyika kuhusiana na dau lililoshinda; wakati mgogoro wa nasibu/bashiri au tuzo unapokua unasuhulishwa; au kwa kipindi ambacho tuzo inabaki pasipo kudaiwa.

7.6.Malipo yoyote yanayofanyika kwa waendeshaji wa mitandandao ya simu (Tigo Pesa, Vodacom Mpesa, na Airtel Money) zitalipwa kutoka kwenye Akaunti yako

7.7. Kodi zozote zinazotakiwa kulipwa kwa Mamlaka Ya Mapato ya Tanzania (TRA) yatakatwa kutoka katika akaunti yako.

8. Kuchezesha bahati nasibu na Namba za Bahati/Ushindi

The Network Ltd itaamua muda, marudio, tarehe na namna ya kuchezesha bahati nasibu katika kila mchezo

8.2. Kila bahati nasibu itachagua namba za bahati/ushindi bila kufuata Utaratibu kwa kutumia kizalishi cha namba bila mpangilio kama kilivyothibitishwa na GBT.

8.3 Kama bahati nasibu/droo itakua imezuiwa kutokana na kifaa kushindwa, au kwa sababu nyingine ile, droo/bahati nasibu itamalizika kwa kufuata taratibu zinazotumika katika bahati nasibu/droo katika mchezo huo. Kama droo/bahati nasibu haiwezi kufanyika katika tarehe au muda uliowekwa, itafanyika mapema iwezekanavyo baadae.

8.4. Kama droo/bahati nasibu yoyote itatangazwa kua ni batili, droo/bahati nasibu nyingine itafanyika kwa kuzingatia taratibu za kuendesha droo/bahati nasibu na kuamua namba za bahati/ushindi.

8.5.The Network Ltd. italipa tuzo kulingana na matokeo yaliyorekodiwa na droo tu kwa mujibu wa kanuni ya 8.4 na ikarekodiwa kielekroniki katika mfumo wa kompyuta wa The Network Ltd. The Network Ltd. haitolipa tuzo kwa matokeo yaliyorekodiwa sehemu nyingine yoyote, ikihusisha kwa mfano katika magazeti, namba za simu au katika tovuti.

8.6. The Network Ltd. haitotakiwa kukulipa namba zozote zilizotangazwa kimakosa kwenye droo/bahati nasibu

9. Taarifa juu ya Washindi

Kama utadai au kulipwa tuzo, utachukuliwa moja kwa moja kua umetoa ruhusa kwa The Network Ltd kua na haki ya kuchapisha, kupitia njia yoyote ya mawasiliano ikiwemo mtandao kwa sababu za kutangaza ushindi, jina lako kamili (pamoja na jina maarufu), mji unaotokea/ishi, picha, na video bila madai yoyote ya kutangaza, kuchapisha au haki nyingine kwa kipindi cha mpaka miezi thelathini na sita tangu siku ya kutolewa tuzo. Pia utaipa The Network Ltd haki ya kuchapisha, kwa kipindi cha mpaka miezi thelathini tangu kipindi cha kutolewa kwa tuzo taarifa yoyote ya nyongeza ambayo utaitoa kwa hiari yako. Hautokua na madai yoyote kwa The Network Ltd kwa kuvamia faragha au kwa sababu nyingine yeyote juu ya kusambazwa au kutangaza jina lako, mahali unapotokea, picha, video au taarifa ulizozitoa kwa hiari yako mwenyewe

9.2. Kama utashinda Tuzo, unaelewa na kukubali kwama The Network Ltd. inaweza, kama itahitajika kisheria, kutoa maelezo juu ya tuzo hiyo kwa mamlaka husika.

9.3 Kwa kujihusisha na mchezo, unaridhia waziwazi kukusanya, matumizi na kutoa kwa The Network Ltd, waajiriwa wake, mawakala au/na watoa huduma, kwa taarifa zako kwaajili ya kufanya na kusimamia mchezo.

9.4. Unakubali kwamba The Network Ltd. in haki ya kukutumia jumbe za promosheni mpaka utakapoamua kujitoa.

10 Kufungwa kwa mchezo n.k.

10.1The Network Ltd inaweza, baada ya kuwasiliana na GBT, kutangaza siku ya kufunga kwa mchezo wakati wowote. Hakuna ingizo kwa mchezo husika litauzwa baada ya kufungwa.

10.2. The Network Ltd inaweza pia (kama itaamua yenyewe) kuzuia kwa muda au kutoa mchezo wowote baada ya kushauriana na GBT

11. Kikomo cha uwajibishwaji kisheria

Pale ambapo itaagizwa na GBT, The Network Ltd (ikiona inafaa- na ikiwa inafanya hivyo kwa sababu za msingi), inaweza kutangaza kwamba bashiri/dau lina dosari. Katika mazingira haya, maingizo husika na zawadi zilizoshinda zitakua batili na The Network Ltd itafanya aidha;

a) Kukupa fursa ya kuweka dau jingine la thamani linganifu na ya awali; au

b) Kurudisha kiasi kilicholipwa kwa dau/bashiri iliyoharibika. The Network Ltd itaamua ipi kati ya (a) au (b) hapo juu kutumika. Hautokua na haki ya kufuta bashiri/dau. Kwa mujibu wa kanuni ya 11.1 (b) na kanuni ya 12.1, hakuna marejesho ya fedha yatakayofanyiwa kwa mazingira yoyote. Hakuna riba itakayolipwa kwa marejesho yoyote.

11.2. Kama The Network Ltd itajiridhisha kua kufutwa kwa bashiri ilisababishwa na udanganyifu, uzembe, au makosa ya The Network Ltd na bashiri itakua lakini kwa kufutwa, ingekua ni bashiri ya ushindi, kwahiyo The Network Ltd haitorudisha gharama ya dau na The Network Ltd itawajibika kulipa kiasi sawa na Tuzo ambayo ungestahili kama bashiri isingefutwa.

11.3. Itakua ni jukumu la The Network Ltd kulipa tuzo kwa wamiliki halali wa bashiri zilizoshinda tu, au kurudisha fedha kadiri ya mazingira yaliyoelezwa katika kanuni hizi. Bila kuathiri kanuni ya 11.1 na 11.5, The Network Ltd haitawajibika kisheria kwa hasara yoyote ile isipokua, kwa mujibu wa kanuni ya 11.4, kutokulipa kwa marejesho ya fedha ambayo unashahili kwa mujibu wa kanuni hizi. The Network Ltd haitakua na wajibu kisheria kwa hasara yoyote ya faida, au hasara ya matokeo uliyoipata (au anayeshikilia au mmiliki wa bashiri, mtu yoyote anaedai tuzo katika kipindi cha madai ya tuzo hiyo au mtu yeyotw) inayotokea kutokana na kujitoa kwenye mchezo au kujihusisha au kutojihusisha katika mchezo wowote. Hii inahusisha hasara, kwa sababu yoyote ile ya nafasi ya kushiriki katika mchezo husika.

11.4 The Network Ltd haitakua na wajibu kisheria kwa mtu yoyote kwa;

a) Matukio yasiyozuilika na yasiyotabirika (mfano vita, migomo, moto, mafuriko, ukame, kukatika kwa umeme, matatizo ya kimtandao, utangazaji au mawasiliano (ya kutumia) simu, redio au televisheni)

b) Kushindwa au kuharibika kwa mfumo wote wa komputa au sehemu yake au rekodi ya The Network Ltd au washirika wake (pamoja na tovuti na/au mfumo wa komputa wa The Network Ltd)

c) Makosa yanayosababishwa na mfumo wote wa komputa au sehemu yake au rekodi ya The Network Ltd au washirika (pamoja na tovuti na/au mfumo wa komputa wa The Network Ltd)

d) Kukawia, hasara, makosa au kukosa kufanya au iliyofanywa na posta au njia nyingine za kuwasilisaha au kwa mifumo ya kibenki;

e) Kitendo kingine au tukio ambalo linazuia kutolewa kwa bashiri halali (ikihusisha kushindwa kwa tovuti kuonyesha kwa usahihi katika kifaa kilichotumika kutazama)

f) Kukataa kuruhusu mtu yeyote kucheza Bahati Nasibu au kumruhusu mtu yeyote kucheza mchezo mtandaoni au kwa nyia ya SMS au Pesa kwa simu ya mkononi

g) Hasara yoyote itakayosababishwa na wewe, pamoja na kutumia vibaya au matumizi yasiyokubalika ya nywila, pesa ulizopoteza kwa kucheza michezo ya mtandaoni au kupitia SMS na kushindwa kutaarifu The Network Ltd mabadiliko ya mawasiliano yako.

h) Hasara yoyote iliyosababishwa na kufeli au kufanya vibaya kwa: kifaa chako au teknolojia; watoa huduma ya mtandao; watoa huduma wa mtandao wa simu za mkononi wa mtu yeyote au mtu wa tatu.

11.5. Hakuna kitu chochote katika kanuni hizi kinachozuia:

(a) mtu yeyote atawajibika kisheria

(i) kwa udanganyifu

(ii) kwa kifo au majeraha yanayosababishwa kutokana na kuvunja wajibu ambao mtu anao wa kuhakikisha ananachukua tahadhari na anafanya jambo kwa ujuzi unaotakiwa

(b) uwajibikaji mwingine wowote ambao hauwezi kuachwa kwa mujibu wa sheria.

11.6. Unakiri na kukubali kwamba hautegemei katika, na hautakua na nafuu kulingana na kauli, uwakilishi, waranti (iwe kwa uzembe au iliwekwa kwa uaminifu) au kuelewa mtu yeyote awe au asiwe sehemu ya kanuni hizi.

12. Migogoro na maamuzi ya The Network Ltd

12.1. Maamuzi ya The Network Ltd juu ya bashiri kua iliyoshinda au laa, au kuhusiana na suala lolote au mgogoro unaotokana na kulipa au kutokulipa tuzo, itakua ya mwisho na yenye kufunga pande zote, lakini tu yapaswa kua maamuzi sahihi (na kwa mujibu wa kanuni ya 12.3). Bila kuathiri sentensi iliyopita na kanuni ya 11.1, kufuatiwa maamuzi yaliyofanywa na The Network Ltd. The Network Ltd itarudisha gharama za bashiri au itabadili bashiri iliyo katika mgogoro na bashiri katika mchezo wa sasa kwa gharama ile ile.

12.2.Nafuu iliyopo katika kanuni ya 12.1 itakua ndio nafuu pekee kwa mchezaji, na marejesho yoyote ya gharama au mabadilishano yatamtoa The Network Ltd kwenye wajibu wake kisheria kutoka kwenye mgogoro huo (kwa mujibu wa kanuni ya 12.3). The Network Ltd hatokua na wajibu wa kulipa riba yoyote kwa mujibu wa marejesho yaliyofanyika chini ya kanuni hii ya 12.

12.3.The Network Ltd inaweza kuzuia malipo ya tuzo au/na kufanya malipo mahakamani mpaka mgogoro utakapokua umetatuliwa.

12.4. Mgogoro wowote wa kisheria utapelewa moja kwa moja katika Bodi ya michezo ya bahati nasibu ya Tanzania (GBT)

13. Kwa ujumla

13.1 Mtu yeyote anayebashiri au anakusanya mkeka kwaajili ya kuhalalisha au anadai tuzo kwa uwezo wowote ule, anakubali kufuata matakwa ya sheria inayohusika, kanuni hizi (vyote kama vinavyofanyiwa marekebisho kadiri muda unavyoruhusu) na kanuni nyingine zozote au taratibu, kauli au maelezo ambayo The Network Ltd inaweza kuyatoa kuhusiana na mchezo huo uliochezwa mtandaoni au kupitia SMS/Fedha kwa njia ya simu ya mkononi.

13.2. The Network Ltd inaweza kubadilisha kanuni hizi, taratibu husika za michezo, na kanuni nyingine za michezo zinazotumika katika michezo inayochezwa mtandaoni na kupitia SMS au pesa kwa njia ya simu ya mkononi wakati wowote. Mabadiliko hayo yataanza kutumika mapema tangu tarehe ya ya kuchapishwa katika tovuti (au mapema itakavyotangazwa na The Network Ltd), au kwa kutoa taarifa kwako kwamba mabadiliko yamefanyika (lile litakalotangulia kati ya haya) na itatumika kwa bashiri zilizochezwa baada ya tarehe ambayo imeanza kutumika, na/au maingizo yaliyoletwa kwako kabla ya tarehe kama inafaa. Taarifa inaweza kua kwa njia ya barua pepe, taarifa kwenye account, posta, au njia yoyote ya mawasiliano ambayo The Network Ltd itaona inafaa. Unakubaliana kwamba utafungwa na mabadiliko utakapocheza tena mchezo unaochezwa mtandaoni au mchezo unaochezwa kwa njia ya SMS au pesa kwa njia ya simu ya mkononi, pale utakapo fungua akaunti yako tena, unapodai tuzo baada ya mabadiliko kufanyika, au (pale inapohusika) pale unapokubali wazi mabadiliko, kwa kile kitakachotangulia kwanza.

13.3 Kama kifungu (au sehemu ya kifungu) au kanuni iliyotajwa hapo juu imeamuliwa na mahakama ya Tanzania kuwa batili na/au haitekelezeki kisheria, maamuzi hayo yataathiri kifungu (au sehemu ya kifungu hicho) na haitafanya vifungu vingine kuwa batili au kutotekelezeka kisheria.

13.4. Hautoweza kutoa au kuhamisha (kwa ujumla wake au sehemu) haki zako na/au wajibu kwa mujibu wa kanuni hizi. Uvunjifu wa kanuni hizi unaweza kupelekea kutumika kwa akaunti yako (pamoja na vifungu vya michezo inayochezwa mtandaoni au kupitia SMS au pesa kwa njia ya simu na/au njia ya kufia tovuti) kufutwa/kuvunjwa mapema na The Network Ltd. The Network Ltd itatoa au itahamisha haki zake na/au wajibu chini ya kanuni hizi kwa ujumla wake au sehemu kwa mtu yeyote wa tatu kwa maamuzi yake binafsi.

13.5. Unakubali kwamba pale utakapo wasiliana na timu ya huduma kwa wateja, utatoa taarifa zinazohusiana na mchezo zinazohitajika na The Network Ltd.

13.6 Faragha: Kampuni itaheshimu faragha yako na itachukua jitihada za makusudi kulinda taarifa zako kwa usiri wa hali ya juu wakati wote. Isipokua, kampuni haitowajibishwa kwa upotevu wa data. Taarifa zako binafsi hazitoweza kutolewa kwa mtu wa tatu isipokuwa: inapohitajika kufanya mchakato wa maombi yako; kwa wajibu au mujibu wa sheria’ kwaajili ya kuutekelezaji wa vigezo na masharti: au kwa kulinda haki au mali ya kampuni. Kumbuka: Taarifa binafsi ulizozitoa zinaweza kutolewa kwa “credit reference bureau” ambao wanaweza kuweka rekodi ya taarifa hizo.

13.7. Ushindi wowote utatakiwa kukatwa kodi kwa kiwango cha 20% ya kiwango tuzo uliyoshinda, kama inavyotakiwa na serikali ya Tanzania.

13.8. Majanga ya Asili: Kampuni haitawajibika kwa namna yoyote ile kwa matokeo ya matukio yaliyo nje ya uwezo wa kukabiliwa/kuzuiwa na kampuni, kama vile, matendo ya kigaidi, migogoro ya kisiasa, vita, majanga ya asili, kuharibika kwa mawasiliano (ya kutumia) simu, redio au televisheni, uvamizi wa kimtandao, udakuzi n.k

13.9.Haki Miliki: Vitu vyote katika tovuti, SMS, huduma za simu, na majukwaa yote ya kielectroniki vinamilikiwa na kampuni, pamoja na washirika wake na wakandarasi na inalindwa na sheria za kimataifa za haki miliki na taratibu zake, pamoja na bidhaa, nembo, alama ya biashara, alama ya huduma, majina ya biashara, n.k. Hakuna sehemu ya tovuti, SMS, au huduma ya simu ya mkononi inaruhusiwa kunakiliwa, kutolewa tena, kutunzwa, kurekebishwa, kuchapishwa tena, kupakiwa kwenye mtandao, kusambazwa kwa namna au jinsi yoyote ile, na haitaruhusiwa kuhusishwa kwenye tovuti nyingine au kwenye mifumo binafsi au ya uma ya kielectroniki ikihusisha maandishi, alama, video, meseji, msimbo, au programu bila ridhaa iliyotolewa kwa njia ya maandishi kutoka kwenye kampuni.

14. Mamlaka ya Kisheria

Makubaliano haya na mahusiano ya kimkataba kati yuako na kampuni yatadhibitiwa na vigezo na masharti haya na yatatafsiriwa kwa mujibu wa sheria husika na inayotumika nchini Tanzania. Na mashitaka yote yatasikilizwa katika mahakama za Tanzania. Pia kama kutakuwa na tatizo la fasiri za kanuni, kanuni za Kiingereza zitapewa kipaumbele

15. Fasili

Akaunti:
akaunti inayomilikiwa na mchezaji kwenye mfumo wa kompyuta wa The Network Ltd. BET Utaratibu wa kuingia kwenye Mchezo

The Network Ltd:
kampuni iliyoanzishwa Tanzania

Mfumo wa kompyuta wa The Network Ltd:

mfumo wa kikompyuta unotumika na au kwa niaba ya The Network Ltd kulingana na mda huska kuendesha michezo ya TATU MZUKA, kusimamia akaunti, kuwezesha maingizo na kulipa Tuzo

GBT:

Bodi ya Michezo ya Bahati Nasibu Tanzania

Kipindi cha Kudai:

kipindi cha muda wa siku 30 baada ya tarehe ya droo.

Kampuni:

The Network Ltd

Timu ya Huduma kwa Wateja:

The Network Ltd itakuwa na simu kwa ajili ya wachezaji, taarifaza mawasiliano ambazo zimewekwa bayana mwishoni mwa kanuni hizi. Rejea kwenye tovuti ya Timu ya Huduma kwa Wateja mda wa kazi.

Droo:

mchakato ambao hutoa matokeo kwenye machaguo yaliyofanywa bila kufuata taratibu na The Network Ltd ya seti za namba za ushindi kwa mchezo

Mchezo uliojikita kwenye droo:

sawasawa na mchezo

Mapumuziko ya droo:

ni kipindi kabla ya droo ambapo hakuna machaguo yatakayoingizwa kwenye droo hiyo.

Hatua za droo:

hatua za droo ambazo zitatumika kwenye droo kama zilivyoamuliwa na The Network Ltd kadri mda unavyoruhusu.

Mchezo:

mchezo wa TATU MZUKA matokeo yake huamuliwa na droo

Mchezo uliochezwa kupitia simu:

mchezo ambao maingizo yake yanaweza kuanzishwa kupitia ujumbe fupi wa maandishi(sms) au pesa kwa njia ya simu au kwa njia nyingine.

Mchezo uliochezwa Mtandaoni:

ni mchezo ambao maingizo yake huanzishiwa/huchezwa kupitia tovuti

Kanuni zilizoainishwa za Mchezo:

Kanuni yeyote iliyotolewa na The Network Ltd ikijumuisha au kama mbadala wa kanuni hizi, ambazo zinatumika kwenye mchezo mahususi unaochezwa mtandaoni

Taarifa zinazohusiana na mchezo:

historia ya muamala wako, historia ya mchezo na taarifa yoyote ambayo The Network Ltd itaitaka kutoka au kuhusu wewe kabla hujapewa fursa ya kucheza mchezo mtandaoni ( ambazo zinaweza kuhusisha, kwa mfano , Jina lako, jina la mtumiaji, nywira, namba ya simu, taarifa za fedha kwa njia ya simu,kadi ya taarifa zako za madeni, taarifa ulinzi, anuani, taarifa za utambulisho, barua pepe, tarehe ya kuzaliwa, na jinsia

Taarifa za utambulisho:

taarifa hizi utumika kukutambulisha, ikiwa ni pamoja na taarifa zinazotakiwa na The Network Ltd kuthibitisha ukweli wa hizo taarifa.taarifa za utambulisho zinaweza kuhusisha hali yoyote ya taarifa inayohusiana na mchezo na taarifa yoyote au hati unazotoa wakati wa kudai Tuzo. Fumu zinazokubaliwa za utambulisho ni: leseni ya udreva, hati ya kusafiria, kitambulisho cha kupigia kura.

Mkeka:

ni mkeka uliyopo kwenye tovuti ambao unaweza kuuchagua kama chaguo lako kwa Bahati Nasibu

Tuzo ya maingiliano:

ni tuzo ambayo mchezaji ameshinda kutokana na ubashiri wake.

Chaguo la bahati:

ni chaguo ya namba ambazo zimechaguliwa bila kufuata utaratibu maalum na mfumu wa kumpyuta wa The Network Ltd kwa niaba yako kwa ajili ya Bahati Nasibu.

Pesa kwa njia ya simu:

Tigo Pesa, Vodcom Mpesa na Airtel Money

PICK 3:

jina mbadala la mchezo TATU MZUKA

Mchezaji:

ana maana sawa na wewe

Sera ya faragha:

sera ya The Network Ltd kuhusiana na kutumia na kutunza taarifa zako binafsi (ikuhusisha lakini sio tu taarifa zinazohusiana na mchezo) ,kama itakavyorekebishwa kulingana na mda muafaka

Tuzo:

tuzo ya maingiliano. Rejea kwenye kanuni hizikwenye Malipo ya tuzo ikijumuisha kutunukiwa tuzo isiyo kuwa na pesa mkononi

Fomu ya kudaia Tuzo:

fomu hutolewa na The Network Ltd inayotakiwa kujazwa na kukusanywa ili kuwa na sifa ya kudaia baadhi ya tuzo kwa mujibu wa kanuni hizi.

Muundo wa Tuzo:

thamani ya tuzo na nafasi ya kushinda kwenye mchezo mmoja kama ilivyopangwa na The Network Ltd na kuwekwa bayana kwenye hatua za mchezo katika mchezohusika.

Hatua:

nyaraka inayotolewa na The Network Ltd kwa mchezo mahususi uliochezwa matandaoni ikiwa ni nyongeza kwenye kanuni hizi, ikijumuisha jina la mchezo, bashiri, jinsi ya kucheza, namna ya kushinda tuzo, tarehe,au idadi ya droo, muundo wa mchezo wa tuzo, namna washindi wa tuzo wanapatikna, na taarifa zingine zinazohusiana na mchezo unaochezwa mtandaoni.

Chaguo:

Seti ya namba zilizochaguliwana nawewe (ziwe zimechaguliwa na wewe au kupitia kuzamisha kwa bahati)

Tovuti:

Tovuti tatumzuka.co.tz

Tiketi:

Uwasilishwaji kwa maandishi au alama wa ubashiri wako.

Namba ya tiketi:

kielelezo cha herufi na namba ikijumuisha kama sehemu ya tiketi ambayo utambua a ni ya kipekee kwenye bashiri mahususi na ambayo imerekodiwa kwenye mfumo wa kompyuta na, kwa maingizo yaliyonunuliwa kwa kutumia akaunti yako, kwenye historia ya muamala wako.

Historia ya muamala:

Historia ya malipo ndani au nje ya akaunti yako, inayoonyeshwa kwenye sehemu ya tovuti “akaunti yangu”

Hatua za kuhalalisha:

Ni maingizo ya The Network Ltd kama yalioainishwa katika kanuni ya 6 au kama itakavyoamuliwa na The Network Ltd kila wakati

Bashiri ya kushinda:

Ni bashiri ambayo inakupa sifa ya kupata tuzo ambayo inakidhi vigezo vyote vya kuhalalisha.

Namba ya bahati:

ni namba au/na herufi zinazotumika kuamua maingizo ya ushindi katika mchezo.

Wewe:

Mmiliki wa akaunti ambaye anasifa ya kununua maingizo kwa kutumia akaunti, na ambaye akaunti akaunti yake haijafutwa, haijafungwa au kusimamishwa.