Jinsi ya kucheza TatuMzuka

  1. Nenda kwenye Mfumo wa Pesa kwenye simu yako, Chagua Lipia Bili kisha namba ya kampuni weka 555111
  2. Kwenye namba ya kumbukumbu, ingiza namba zako Tatu za bahati kuanzia 0-9 zikifuatiwa na neno WEB, mfano 637 WEB
  3. Ingiza kiasi chochote cha fedha kama dau lako. Unaweza kuweka kiasi chochote kuanzia Sh 500 hadi 30,000

Nawezaje kuingia kwenye Jackpot?

Habari, Kila unapocheza unapata nafasi moja ya kuingia kwenye Jackpot. Ahsante

Nimepatia namba zote lakini nimepewa mara mbili ya dau langu

Habari, Ili kushinda mara 200 inabidi namba zako za bahati zilingane katika mpangilio sawa na namba za ushindi toka TatuMzuka, namba zako hazikuwa katika mpangilio sawa na namba za droo. Karibu sana

Baada ya namba zangu tatu naandika nini?

Habari, Unatakiwa kuandika neno au kituo ambapo umesikia au kuona Tangazo la Tatumzuka. Ahsante

Kwanini ujumbe wa Tatumzuka unachelewa kunifikia baada ya kucheza?

Habari,Ujumbe wa Tatumzuka utachelewa kukufikia kutokana na mtandao kuzidiwa kugawa ujumbe kwa wachezaji wote wa lisaa husika. Ahsante

Je natakiwa kucheza namba za bahati hizo hizo pekee bila kubadili.

Habari, Unaweza kubadili namba za bahati kila unapocheza Tatumzuka ndani ya lisaa. Ahsante

Nafasi ya Kushinda Tatu Mzuka

Linganisha namba 2=nafasi ya kupata ni 1 kati ya 6.7

Linganisha namba tatu Kwa mlolongo nafasi ya kupata ni 1 kati ya 1000

Naweza kucheza mara ngapi kwa siku

Habari, unaweza kucheza mara nyingi kadri uwezavyo kwa saa au kwa siku. Ahsante

Je naweza kujua nina point ngapi hadi sasa

Habari, Bahati nasibu ya TatuMzuka huchezeshwa kwa kutumia namba za bahati pamoja na tiketi na sio point. Ahsante

TatuMzuka itaisha lini?

Habari, TatuMzuka ni mchezo wa bahati nasibu endelevu na hauna kikomo. Ahsante

Mwisho wa kucheza ni saa ngapi?

Habari, TatuMzuka huchezwa kwa saa 24. Ahsante

Je napataje namba za bahati?

Habari, Pangilia namba zako kwa kukisia kichwani kuanzia 0 mpaka 9 ili kubahatisha namba za ushindi. Ahsante

Nimecheza mara nyingi lakini sijawahi kushinda kwanini?

Habari, Ili kushinda unapaswa kubahatisha namba za ushindi zote tatu kwa mpangilio au kubahatisha mbili kati ya Tatu za ushindi. Ahsante

Kwanini mtu asiongezewe kiwango kama atafananisha namba zote tatu lakini hazipo kwenye mpangilio?

Habari, Ni utaratibu ili upate mara 200 ya pesa lazima namba zako za bahati zifanane sawa kwa mpangilio na namba za ushindi wa lisaa husika. Ahsante